Wadudu Waharibifu Leucaena psyllid
Gerry D. Hertel, USDA Forest Service - Forest Health and Management
1998. The Entomology and Forest Resources Digital Information Work Group,
College of Agricultural and Environmental Sciences and Warnell School of Forest
Resources, The University of Georgia, Tifton, Georgia 31793 U.S.A.
BUGWOOD 98-201
 |
|
Wadudu waharibifu wanaoshambulia miti aina ya leucaena waitwao
leucaena psyllid
wamo katika kundi la wadudu lijulikanalo na wengi kama chawa wanaorukaruka wapatikanao
katika mimea. Asili yake ni Amerika ya Kati na Amerika
Kusini, chimbuko la miti ya
leucaena. Mdudu huyo hata akiwa mkubwa
hawezi kuonekana kwa macho. Ana urefu wa karibu milimita mbili na rangi ya
manjano.
Hutaga mayai katikati ya majani yanayochipuka kwenye ncha ya
mti. Mayai huchukua
muda wa kati ya siku 10 na 12 kuwa funza,
viluwiluwi na hatimaye mdudu aliyekomaa.
Mdudu huyo hupatikana sana kwenye miti michanga ya leucaena
ambapo mayai, viluwiluwi wasio na mabawa na wadudu waliokomaa wenye mabawa hupatikana kwa
pamoja. Barani Afrika, mdudu huyo hupatikana katika maeneo ambapo miti aina ya
leucaena
hukuzwa, hasa katika Burundi, Ethiopia, Kenya, Malawi, Mauritius,
Msumbiji, Reunion,
Tanzania, Uganda na Zambia.
Jamii ya miti ya leucaena
ina aina karibu 10 tofauti za mmea huo. Ni mti ambao una matumizi
mengi. Ingawa
njia thabiti kukabiliana na mdudu huyo mharibifu haijapatikana, wakulima na watu wenginc
waliopanda leucaena
hawafai kuing'oa kwa sababu kinga kamili inatafutwa bado. Wadudu wawezao kumla mdudu huyo
anayeharibu leucaena wanatathminiwa. Kadhalika, aina ya miti ya leucaena
isiyoweza kuharibiwa na wadudu hao inachunguzwa. Ye yote anayegundua kwamba mdudu huyo
amerahibu mimea hiyo anaweza kuripoti na atasaidiwa ipasavyo akiwasiliana
na:
Kwa sababu si rahisi kumwona mdudu huyo kwa macho,
hudhihirika yupo madhara aliyoyasababisha mitini yakianza
kuonekana. Wadudu waliokomaa
pamoja na viluwiluwi hudhuru miti ya leucaena kwa kufyonza utomvu kutoka kwa miti na
matawi yanayochipuka, majani na maua.
Matokeo yake huwa ni kudhoofika na kukwajuka kwa majani. Kwa
kawaida, majani kwenye
mimea inayochipuka yakivamiwa, huharibiwa kabisa. Wakati
mwingine, wadudu hao
husababisha kukauka kabisa kwa mmea wanaouvamia.
|
| Wadudu wanaoharibu leucaena |
 |
| Mayai ya leucaena psyllid yakiwa mtini |
 |
 |
| Mti ulio na leucaena psyllid |
Ramani inayoonyesha jinsi leucaena psyllid walivyoenea kutoka Amerika
Kaskazini hadi Afrika kutoka 1984 hadi 1992 |
Maelezo yametayarishwa na Gerry Hertel wa USDA Forest Service, yametolewa na
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na kuchapishwa na Forest Health
Management Centre SLP 30241 Nairobi
Photo Credits: W. Nagamine, FAO Archives and W. M. Ciesla
|